Nafasi za kazi kwa walimu wapya na waelimishaji katika elimu ya Awali utotoni
Serikali ya Victoria imetoa dola bilioni 14 kupanua programu za chekechea kote jimboni. Katika muongo(miaka kumi) ujao Victoria itahitaji maelfu ya walimu na waelimishaji wa shule za awali utotoni.
Elimu ya Awali Utotoni inaleta mabadiliko katika maisha ya watoto na familia. Walimu wa Awali Utotoni na waelimishaji kutoka asili tofauti za kitamaduni na lugha wanafanya mabadiliko zaidi.
Wafanyikazi wanaozungumza lugha mbili na wenye tamaduni mbili katika huduma za watoto wachanga husaidia kufanya programu za chekechea kufikiwa zaidi na familia kutoka asili tofauti za kitamaduni na lugha na kuakisi jumuiya za tamaduni nyingi ndani ya jimbo.
Kufanya kazi katika elimu ya awali utotoni hutoa faida nyingi. Inatoa fursa ya:
- kuleta mabadiliko na kuboresha matokeo kwa watoto na familia zao
- kusaidia watoto kukua na kujifunza katika miaka yao ya mapema
- fanya kazi katika nyanja ambayo ni za kuridhisha na zenye ubunifu.
Msaada wa kifedha:
Kuna chaguzi mbalimbali za masomo na usaidizi wa kifedha unaopatikana kwa watu wanaotaka kuwa walimu au waelimishaji wa elimu ya wali utotoni.
Kwa habari zaidi kuhusu taaluma katika elimu ya awali utotoni na usaidizi wa kifedha kwa masomo nenda kwa Become an early childhood teacher or educator
Ajira:
Ajira katika elimu ya awali utotoni inasimamiwa na wasimamizi wa huduma binafsi na watoa huduma wa programu za chekechea.
Nenda kwenye Early Childhood Jobs website ili kuona ni kazi zipi zinazopatikana na kusoma baadhi ya mifano ya watu wanaofanya kazi katika sekta hiyo.
Updated