Kuhusu Nyenzo za Shule ya Chekechea
Kwa watoto, kucheza na kujifunza huenda pamoja. Kucheza ndivyo jinsi watoto wanavyojitambua na kujielewa na kuelewa ulimwengu wao. Wazazi, walezi na familia ni sehemu kuu ya safari hiyo. Kila kitu katika Zana yako ya Nyenzo za Shule ya Chekechea za mtoto wako kimeundwa ili kushirikiwa na kufurahiwa kama familia.
Katika shule ya chekechea, Mfumo wa Masomo na Ukuaji wa Watoto wa Victoria (VEYLDF, Victorian Early Years Learning and Development Framework) hutumiwa kubuni hali za masomo zinazomsaidia mtoto wako kukua na kustawi katika sehemu tano za masomo na ukuaji. Sehemu hizi tano matokeo ni:
- Utambulisho
- Masomo
- Jamii
- Mawasiliano
- Ustawi
Sanduku la shughuli
Sanduku la shughuli si kesi tu ya kubeba vitabu na midoli. Inaweza kutumika kusaidia kujifunza na maendeleo kwa njia nyingi.
- Chukua sanduku la shughuli kwa pikiniki au matembezi na marafiki na familia
- Mkeka wa unga wa kuchezea
- Chombo cha kuchezea
Je, wajua? Kasha la shughuli za Zana limeundwa kuwa bidhaa inayofaa kwa mazingira. Imetengenezwa kwa nyenzo zilizorejelewa inapowezekana na inaweza kutumika tena kuhifadhi hazina za mtoto wako. Kunja Zana iwe bao la mchoraji au weka Zana ilalazwe ili nyuso ya kijani kibichi itumike kwa mchezo wa kufikiria.
Chaki, ubao na dasta
Ubao na chaki ni nzuri kwa ubunifu na kukuza ustadi mzuri wa kutumia misuli midogo wakati watoto wanashika chaki. Ubao unaweza kutumika kama kitu cha kuchorea kwa chaki na pia kinaweza kutumika kutengeneza maumbo kwa unga wa kuchezea.
- Tafuta mahali nje na chora kile unachokiona karibu nawe
- Tumia chaki kuunda ulimwengu kutoka kwenye mawazo yako
- Jizoeza kuandika jina lako
- Tumia koala kwenye dasta kuunda sanaa ya kusugua. Weka koala chini ya karatasi na kusugua kidogo na chaki
Je, wajua? Dasta ya chaki ina plastiki iliyosindikwa iliyobaki kutoka wakati pesa za Australia zinatengenezwa.
Mbegu
Kupanda mbegu na watoto ni hali ya kujifunza yenye ushahidi mwingi wa kisayansi inayowaruhusu kuona maajabu ya ulimwengu wa asili. Watajifunza juu ya mazingira asili, kukuza lugha na kujifunza kufuata maelekezo rahisi. Watajifunza pia jinsi ya kuchunguza mambo baada ya muda.
- Zungumza kuhusu mimea na utaje majina ya sehemu zake
- Ipande pamoja nao
- Jifunza kuhusu mzunguko wa maisha ya mimea
- Taja matunda na mboga kwenye maduka
Je, wajua? Alfalfa ni kunde kutoka kwenye familia ya njegere na ina vitamini na madini mengi. Majani ya mmea yanapoumizwa hutuma ishara kwa nyigu ambayo huwaambia wausaidie kuchavusha tena. Unaweza hata kuitumia katika kupika kwako!
Kushona picha za wanyama
Miaka ya utotoni ni wakati ambapo watoto huanza kudhibiti zaidi misuli midogo ya mikono, vidole, vifundo vya mikono, miguu na vidole vya miguu. Kukuza misuli midogo ya mikono na vidole ni muhimu kwa watoto kujitunza na baadaye, kwa kuandika. Mtoto wako anaweza kukuza ujuzi wa matumizi ya misuli midogo kwa kutumia udongo wa kuchezea, penseli za rangi au kushona wanyama na baadaye, kwa kuandika. Zifuatazo ni baadhi ya njia unazoweza kutumia kama mazoezi ya ujuzi wa kutumia misuli midogo:
- Pitisha uzi kwenye mashimo ya mnyama
- Fungua na funga kisanduku cha shughuli
- Fanya mazoezi ya kufunga zipu au vifungo
- Viringisha udongo wa kuchezea kwa mikono na vidole
Je, wajua? Kamba za viatu zimetumika tangu karibu miaka 3000 BC kufunga ngozi kwenye miguu.
Fumbo (puzzle) la ramani ya Australia
Mafumbo rahisi humsaidia mtoto wako kukuza uvumilivu, umakini, utatuzi wa shida na ustadi wa kutumia misuli midogo. Mtoto wako anapoingiliana na fumbo, hufanya uchaguzi, kutambua maumbo na kutumia kumbukumbu zao.
- Jizoeza uthabiti kwa kutumia majaribio na makosa ili kukamilisha fumbo
- Zungumza kuhusu wanyama
- Chunguza kwa zamu
- Wahimize watoto kuzungumza kuhusu maumbo na kama yanalingana
Je, wajua? Echidna na platypus ndio mamalia pekee ulimwenguni ambao hutaga mayai.
Penseli ya Rangi na Pedi ya Kuchora
Kuchora kwa kutumia penseli ya rangi hutoa njia nyingi za kujifunza:
- kuboresha ujuzi wa matumizi macho, vidole na mikono kama vile kushika penseli
- uratibu wa jicho na mkono
- kujifunza kuhusu rangi na maumbo
- kuonyesha ubunifu na karatasi na nyenzo zingine.
Muhimu zaidi, watoto watajifunza kujieleza kwa usalama na kwa ujasiri. Watoto wengine wanaweza kuwa wanachora alama ambazo huzifahamu na hiyo ni sawa. Huu ni mchakato wa asili wa kujifunza kuchora na kuandika.
- Tumia Pedi ya Kuchora ili kuibua mawazo
- Himiza hali za kuchora kama familia
- Zungumza unapochora
- Taja rangi na maumbo
Je, wajua? Kalamu za rangi zimetengenezwa kwa nta ya nyuki, ambayo hutoka kwa sega la asali lililotengenezwa na nyuki wa Victoria. Nyuki wakiwa kwenye bustani na kupata kitu ambacho ni muhimu kwa familia yao hurudi kwenye mzinga na kucheza densi ndogo ya kufurukuta.
Vitikisa vya Umbo
Kuunda muziki ni njia ya kufurahisha kwa watoto kujifunza maneno mapya, kuimba nyimbo, kujifunza kuhesabu na kujisikia vizuri kujihusu. Kucheza densi, kuimba, kusonga na kurukaruka yote ni sehemu ya burudani. Yafuatayo ni baadhi ya mawazo ya kufurahia muziki na mtoto wako:
- Jaribio la kutengeneza midundo tofauti
- Cheza densi, sogeza na jitikisa kwa wimbo unaoupenda
- Hesabu mapigo
- Tumia nyimbo au mashairi ili kujenga msamiati wa mtoto wako
Je, wajua? Tamaduni nyingi zinaamini kutumia vijiti vya mvua kama chombo cha muziki kunaleta mvua wakati wa ukame.
Udongo wa kuchezea
Mtoto wako anapotumia udongo wa kuchezea kuunda vitu, anafanya mambo mbalimbali muhimu sana:
- kuboresha ujuzi wa matumizi ya misuli ya mikono na vidole
- kutumia hisia zake kutambua vitu
- kwa kutumia mawazo yake.
Kuunda vitu kwa kutumia udongo wa kuchezea ni sehemu muhimu ya kujifunza kwa mtoto wako.
- Viringisha udongo uwe kama mpira, ugonge kwa mikono, uponde kwa mikono, ukande
- Tumia koala kwenye dasta kama muhuri
- Ongeza vitu vingine kama vile vijiti au manyoya au maganda
- Tengeneza mitindo kwa kutumia kitu unachoweza kupata
Je, wajua? Udongo wa kuchezea ni rahisi kuutengeneza nyumbani na kuna mapishi mengi kwenye intaneti. Tengeneza udongo wako mwenyewe wa kuchezea kwenye shughuli ya kufurahisha ya kujifunza ili kufunza kila kitu kuanzia kwa hesabu ya watoto hadi sayansi ya limbukeni.
Vitabu vya watoto
Kusoma vitabu pamoja ni njia nzuri ya kuungana na kukaa pamoja kama familia. Ni mojawapo ya njia muhimu zaidi za kusaidia kukuza hali ya kujua kusoma na kuandika. Kusimuliana hadithi mara kwa mara na mtoto wako kutaboresha mawazo yake na msamiati.
- Chagua kitabu pamoja
- Tafuta mahali pazuri pa kukaa na kusoma
- Umwache afungue kurasa
- Tumia sauti tofauti kwa wahusika, zungumza kuhusu picha
Je, wajua? Kuna thamani kwa kusoma kurudia kusoma vitabu mara kwa mara na si tu kuzingatia hadithi. Uliza mtoto wako kuhusu kitu anachoona, zungumza kuhusu picha na uulize ‘Je, ni nini kitakachotokea baadaye?’
Vikaragosi vya vidole
Vikaragosi vya vidole vinaweza kuwasaidia watoto kufahamu lugha, kuchunguza hisia, na kujifunza njia wanavyoweza kuzidhibiti kupitia mchezo wa kuigiza. Kusimulia hadithi na igizo dhima ni sehemu muhimu ya jinsi watoto wanavyofahamu ulimwengu na wao wenyewe.
- Taja wanyama kwa Kiingereza na lugha zingine
- Tengeneza wahusika
- Tengeneza hadithi
- Tumia vikaragosi ndani na nje
Je, wajua? Unaweza kuunda sauti tofauti kwa kila kikaragosi, na kuifanya iwe njia ya kufurahisha ya kufurahia mchezo wa kibunifu.
Kusawazisha vito
Vito vya kusawazisha vinahimiza mchezo wa ubunifu. Inapotumiwa kuweka na kujenga, pembe tofauti na maumbo ya vito hukuza utatuzi wa matatizo, ufahamu wa anga na ujuzi mzuri wa matumizi ya misuli midogo.
- Jenga peke yake au changanya na matofali mengine na katoni
- Fanya mazoezi ya subira wakati wa kuweka vito. Ikiwa vitaanguka, vuta pumzi 3 na jaribu tena
- Tumia mawazo yako kuunda ulimwengu tofauti na vito
- Chunguza lugha ya maelezo kuhusu umbo, ukubwa na rangi
Je, wajua? Vito kama vile garnet, topazi na zircon vimepatikana huko Victoria.
Kujenga Jamii
Victoria ni jamii yenye watu mbalimbali, nyumbani kwa tamaduni nyingi na lugha tofauti zinazozungumzwa. Utofauti ni sehemu muhimu ya maisha yetu. Vitu vilivyo kwenye Zana vinaendeleza mazungumzo kuhusu jamii mbalimbali. Kwa watoto, kucheza na kujifunza huenda pamoja. Kucheza ndivyo jinsi watoto wanavyojitambua na kujielewa.
- Tumia udongo wa kuchezea ili kujifanya unatengeneza chakula cha tamaduni zingine au utamaduni wako.
- Cheza na Vitikisa vya Umbo wakati unaposikiliza muziki wa jadi kutoka kwenye tamaduni zingine au utamaduni wako
- Zungumza na mtoto wako kuhusu nchi nyingine na wanyama wake wa asili
Je, wajua? Unaweza kufikia miongozo katika lugha nyingi hapa: vic.gov.au/kinder/translations(opens in a new window).
Vitabu vya Kiauslani
Vitabu vyote vilivyojumuishwa kwenye Zana ya Nyenzo za Shule ya Chekechea ya 2024 vina tafsiri za Kiauslani. Unaweza kutumia msimbo wa QR ulio hapa chini ili kuunganishwa kwenye video za vitabu. Kiauslani na manukuu yamejumuishwa kwenye video pia.
Kiauslani ni lugha ya ishara inayotumiwa na idadi kubwa ya jamii ya Viziwi ya Australia na pia ni sehemu ya Mpango wa Lugha za Watoto wa Victoria unaopatikana katika baadhi ya Shule za Chekechea za Watoto wa Umri wa Miaka Minne.
Wataalamu wa elimu wametambua kuwa kuna manufaa mengi kwa watoto kujifunza kwa lugha nyingine wakiwa na umri mdogo, ikijumuisha:
- kukuza ujuzi wa kabla ya kusoma na kabla ya kuandika
- wepesi wa kutambua mambo
- kukuza hali ya kujiamini na ustawi
- kuimarisha hali ya kujitambua.
Bonyeza kiungo hiki kutazama video za usomaji wa vitabu ambazo zinajumuisha Auslan na maelezo mafupi.
Je, wajua? Serikali ya jimbo la Victoria inatoa fedha za ziada kwa watoto wa shule za chekechekea zinazoshiriki ili kuajiri mwalimu wa lugha aliyehitimu ili kutoa mafunzo ya sehemu ya mpango wao wa Shule ya Chekechea ya Watoto wa Miaka Minne kwa lugha nyingine bila wazazi kutozwa gharama yoyote. Pata maelezo zaidi katika: vic.gov.au/early-childhood-language-program.
Ustawi na msaada wa ziada
Watoto wote hujifunza kwa njia tofauti na kwa utaratibu wao wenyewe. Zana ya Nyenzo za Shule ya Chekechea inampa mtoto wako vitabu na vitu vya kuchezea ambavyo vinaweza kutumika kwa njia nyingi tofauti ili kushughulikia uwezo wote. Ikiwa unafikiri kuwa wewe au mtoto wako atahitaji msaada wa ziada, kuna njia kadhaa unazoweza kupata msaada:
- Walimu wa shule ya chekechea wa Victoria wana ujuzi na maarifa ya kusaidia. Zungumza na mwalimu wa mtoto wako kuhusu masuala ya mtoto wako
- Weka miadi ya kuonana na daktari wako au muuguzi wa afya ya uzazi na watoto ili kuzungumzia masuala yako
- Wasiliana na Parentline kwa nambari 13 22 89 kwa ushauri na msaada wa siri bila malipo
Je, Unahitaji Msaada? Ili kupata maelezo zaidi kuhusu aina za msaada zinazoweza kupatikana kwa mtoto wako nenda kwenye: www.vic.gov.au/kindergarten-programs-and-initiatives. Unaweza pia kuomba mwalimu wako wa shule ya chekechea ushauri wa ziada kuhusu msaada unaofaa kwa mtoto wako.
Kuheshimu utambulisho
Tamaduni za Asili ni sehemu muhimu ya historia ya Australia. Kuhimiza watoto wote kujifunza kuhusu tamaduni zote hujenga ufahamu, kukubali na fahari. Tamaduni za Waaboriginal na Torres Strait Islander zinaishi na kustawi leo, na tunajivunia kuzisherehekea kama waandishi na wasanii katika Zana hiii. Zifuatazo ni baadhi ya shughuli zinazomsaidia mtoto wako kujifunza zaidi kuhusu mila na tamaduni za Wenyeji wa Asili.
- Jifunze alama za Asili kwa vitu au wanyama
- Zungumza kuhusu viongozi wa Asili, magwiji wa michezo au wasanii
- Pata maelezo zaidi kuhusu tamaduni na watu wa Asili
Je, wajua? Tovuti ya Victorian Aboriginal Education Association Inc. ina shughuli za kufurahisha, zinazohusisha na kuchunguza mila na tamaduni za Asili. Tembelea tovuti kwa: vaeai.org.au.
Mchoro wa Aboriginal
Ni wakati wa usiku kwenye Gunditjmara Mirring (Nchi). Mwezi na nyota nyingi hung'aa angani.
Alama za karrayn (kangaroo) zimetawanyika kote Mirring. Wakati mwingine unaweza kuona karrayn akirukaruka au kula nyasi.
Weengkeel (koala) yuko macho na ameshikilia tawi la mti mwekundu wa gum. Mti huu ulitumiwa kuunda vitu kama ngao, mitumbwi na kontena ya asili.
Ardhi, anga, maji na wanyama ni muhimu. Kumbuka kuwaheshimu.
Nakia Cadd ni mwanamke wa Gunditjmara, Yorta Yorta, Dja Dja Wurrung, Bunitj, Boon Wurrung na Taungurung. Nakia ni mama, msanii na mfanyabiashara mdogo wa 'More than Lines' na ana shauku ya kuonyesha na kushiriki hadithi kupitia sanaa.
Uliza: Je, ni Wamiliki wa Jadi wa nchi unayoishi, kujifunza na kucheza? Wakati unapokuwa nje, unaona nini, unanuka na unasikia nini?
Updated